Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo ametoa pongezi kwa Kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’ hapa nchini kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye ubora vijijini.
Mh. Jafo ametoa pongezi hizo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe ambapo alifanikiwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi Mitengwe, Kitonga Mango, Boga, mapoja na kituo cha Afya Maneromango.
Aidha Jafo alieza kuwa ujenzi huo umetumia utaratibu huo wa ‘Force Account’ ambapo miundombinu mbalimbali imejengwa kwa gharama nafuu pamoja na kutoa ajira kwa mafundi wanaopatikana katika maeneo miradi hiyo inapotekelezwa.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kukagua jengo jipya la upasuaji, maabara, wodi ya kinamama, nyumba ya daktari, jengo la kuhifadhi maiti, vyumba 12 vya madarasa mapya, matundu ya vyoo 30, pamoja na Ofisi za walimu 3.
Hata hivyo Jafo amewataka wananchi wote nchini kushiriki kulinda na kusimamia rasilimali fedha zinazopelekwa katika vijiji vyao kwaajili ya maendeleo
No comments:
Post a Comment