Nyumba
ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila imechomwa
moto katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi, ambapo askari
mmoja aliuwa.
Tukio
hilo limetokea Desemba 25, 2017, ambapo taarifa zinasema kuwa waasi wa
kundi lijulikanalo Mai Mai walijaribu kuiba mali kutoka makazi hayo ya
rais yaliyoko eneo la Musienene, katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Wakati
wa tukio Rais Kabila hakuwa kwenye nyumba hiyo ambayo iko kijijini
maili 1,680 Mashariki mwa mji wa Kinshasa, huku kundi la Mai Mai na
kundi la waasi wa ADF wakiwa washukiwa wa kwanza juu ya tukio hilo.
Hivi
karibuni Rais Kabila amekuwa akipingwa na wanasiasa mbali mbali kwa
kitendo chake cha kutaka kugombea nafasi ya urais kwa muhula mwingine.
No comments:
Post a Comment