Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezidi kumomonyoka baada ya
wanachama wao zaidi 1,200, wakiwemo viongozi wakuu wa Wilaya ya
Ngorongoro, kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Miongoni
mwa viongozi waliohama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa
Wilaya Ngorongoro, Samweli Ole Nakumbale, aliyekuwa mgombea ubunge wa
jimbo hilo mwaka 2015, Elias Ngorisa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza
la Vijana (BAVITA) Wilaya ya Ngorongoro, Wiliam ole Telele.
Wakizungumza
baada ya kuomba kurudi CCM na kupokewa wakati wa uzinduzi wa kampeni za
CCM za ubunge katika Jimbo la Longido juzi, walisema kuwa ubinafsi
ndani ya Chadema umekithiri na vyeo katika chama hicho hutolewa kwa
kuangalia sura na ukabila.
“Nilikuwa
kada wa CCM nikachukuliwa na mafuriko ya mwaka 2015 nimekaa huko hakuna
kipya ni usanii mtupu. Chama hakina hata ofisi ya wilaya kwenye baadhi
ya mikoa lakini baada ya kulinganisha nikaona kweli nimepotea njia,”
alisema Nakumbale.
Naye
Ngorisa alisema mwanaume mwenye busara, ni yule anayejitafakari na
kujitathimini katika maamuzi yake. “Nimekaa nimetafakari kwa kina,
nikaona kweli kuna mahali nilikosea na ndiyo maana nikaamua kurudi CCM,
kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa vitendo na wananchi wanafurahia
utendaji wa Rais John Magufuli”.
Alisema
kibaya zaidi amekuwa akiandikwa vibaya kila siku kwenye mitandao ya
kijamii kwa mambo ya uongo na uzushi yasiyokuwa na tija, hali ambayo
imemfanya arudi CCM.
“Nimetuhumiwa
sana kwenye mitandao nikiitwa msaliti wakati si kweli, lakini sasa
kutokana na tuhuma zao ambazo hazikuwa na mashiko nimeamua kurudi CCM.
“Nimekuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa miaka 10 kupitia
CCM na ukweli kuna mahali tulikosea baadhi ya viongozi, tulikuwa na
maslahi binafsi badala ya kuhangaika na kero za wananchi, lakini Mungu
ametupa Rais mzalendo aliyejitoa sadaka kwa ajili ya kupambana na
mafisadi na kusimamia rasilimali za nchi,” alisema.
Kwa
upande wake, mfanyabiashara maarufu katika Wilaya ya Longido ambaye pia
ni Laigwanani wa mila ya jamii ya Kimasai, Eliya Malari alisema wazee
wa mila walilala kwake siku 10 wakimuomba arudi CCM, na baada ya
kutafakari utendaji wa Rais Magufuli, alikubali ombi la wazee hao na
kuamua kurudi CCM na wafuasi wake
No comments:
Post a Comment