Beki
na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannnavaro’, amenyoosha mikono juu
na kutamka kuwa inatosha na sasa ataitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja
pekee.
Kauli
hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya timu hiyo kumsajili beki wa
kati Mkongo, Fistoni Kayembe kwa mkataba wa miaka miwili.
Cannavaro
anapambania nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mabeki wanne
ambao ni Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’
na Mkongo huyo.
Cannavaro
alisema anaamini muda wake wa kucheza umefikia kikomo, hivyo ni wakati
wa kustaafu kucheza kwa ajili ya kuwaachia vijana wengine wanaochipukia
kuonekana.
Cannavaro
alisema, akiwa anaendelea kuitumikia Yanga, anasubiria kozi ya makocha
ya hatua ya awali ianze ili na yeye aanze mafunzo kwa ajili ya maisha
yake ya badaye.
Aliongeza
kuwa, amepanga kufanya kazi hiyo ya ukocha kutokana na maisha yake yote
kuhusisha soka, hivyo hataki kutoka nje ya soka zaidi ya kujiongezea
elimu.
“Kiukweli muda wangu wa kuendelea kuichezea Yanga umebaki mdogo na nilichopanga ni kuitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee.
“Mara
baada ya kuachana kuichezea Yanga, basi ndiyo itakuwa mwisho wangu wa
kucheza soka na badala yake nitastaafu kabisa na kuingia kwenye kazi ya
ukocha,” alisema Cannavaro.
No comments:
Post a Comment