Pages

Sunday, December 24, 2017

Korea Kaskazini: Vikwazo vipya ni kama vita

The test of North Korea's Hwasong-15' intercontinental ballistic rocket. File photo 
Korea Kaskazini imetaja vikwazo vya hivi majuzi vya Umoja wa Mataifa dhidi yake ni kama vita.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema kuwa hatua hizo zilikuwa ni kubwa na ngumu kwa uchumi kwa mujibu wa shirika la KNCA la Korea Kaskazini.
Iliongeza kuwa kuwa kuongeza msimamo mkali zaidi wa Korea Kaskazini ndilo jibu kwa Marekani.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lilitangaza vikwazo vipya siku ya Ijumaa kufuatia majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.
Marekani ilipendekeza vikwazo hivyo na kuungwa mkono na wanacha wote 15 wa baraza la usalama la Umoja Mataifa vikiwemo vya kukata mauzo ya mafuta kwa asilimia 90 kwa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini tayari iko chini ya vikwani kutoka Marekani, Umoja wa Mataifa na EU.

No comments:

Post a Comment