Pages

Sunday, December 24, 2017

Mbarawa: Ukitozwa Nauli Isiyo Rasmi Ripoti Vyombo Husika

WaziriI wa Kazi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, pamoja na kuwatakia Watanzania heri ya sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya ameagiza pia kuwaripoti mara moja kwa vyombo husika watu wanaowatoza nauli  isiyo rasmi na kuwataka wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini barabarani.

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter,  akisema ipindi hiki cha sikukuu kimekuwa na changamoto kubwa za usafiri, ikiwemo kutozwa nauli ya juu, na kuwataka kutoa taarifa mara moja kwa vyombo husika.

“Napenda kuwatakia Watanzania wote kila la kheri katika msimu wa sherehe za Xmas & mwaka mpya 2018,wito wangu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri ni kuzingatia sheria na kanuni za barabarani, kwani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu kumekuwa na changamoto ya usafiri,  hivyo kwa abiria endapo utatozwa nauli za juu ya viwango vilivyowekwa usisite kuripoti kwenye vyombo husika kwa wakati”, ameandika Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni kumekuwa na tatizo la wamiliki wa vyombo vya usafiri kuongeza nauli kutokana na wingi wa watu wanaofanya safari zao kuelekea mikoani kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kusababisha ugumu wa usafiri.

No comments:

Post a Comment