Na Saleh Ally
KOCHA
Joseph amefutwa kazi katika kikosi cha Simba na uongozi wa klabu hiyo
ukaendeleza uungwana wake wa kusema wamekubaliana kuvunja mkataba, hii
haina tofauti na ile hali aliyoondoka nayo Kocha Msaidizi, Jackson
Mayanja raia wa Uganda ambaye ilielezwa “ameomba”.
Kuondoka
kwa Omog ni baada ya Simba kulazwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti
dhidi ya timu ya Green Worriers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
Kipigo pekee si jambo linalowaumiza Simba, badala yake ni maumivu ya
kuvuliwa ubingwa.
Huenda
hata kuondoka kwa Kocha Joseph Omog inawezekana ikawa si maumivu ya
Wanasimba wote, ni maumivu ya mwanachama maarufu zaidi wa Simba, Mohamed
Dewji ambaye aliandika mtandaoni kuhusiana na msimamo wake baada ya
Simba kuvuliwa ubingwa akisema hana nguvu kwa kuwa ni mwanachama wa
kawaida na kama ni mawazo, basi anamuomba Omog apumzike.
Haikupita
zaidi ya saa moja, Omog tayari alikuwa katika matatizo na saa moja
baadaye akaondolewa na kuondoka kwake kumebaki kukiwagawa Wanasimba
wengi, wapo wanaokubali na wanaopinga na hili limekuwa ni jambo la
kawaida.
Lengo
la kumuondoa Omog ni kufanya vizuri, kocha huyo anaondoka akiwa na
rekodi nyingi ndani ya misimu miwili na ushee ndani ya kikosi hicho.
Kwani baada ya miaka minne ya kusota ndiye aliyeirudisha katika michuano
ya kimataifa baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho ambalo leo limeng’oa
Simba.
Achana
na rekodi yake akiwa Azam FC kuchukua ubingwa bila ya kufungwa hata
mechi moja, aliiongoza Simba mechi tisa bila kuruhusu hata bao moja na
akashika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga akiwa nao pointi sawa,
wao wakichukua ubingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Lakini
hata wakati anaondoka kikosi cha Simba kipo kileleni, hivyo unaweza
kusema ni kocha aliyetupiwa virago akiwa na kumbukumbu nzuri na
alichokuwa anakifanya na hakuna ubishi, siku chache zijazo, Simba
“watamkumbuka”.
Unaweza
kujiuliza maswali mengi, kwamba kufukuzwa kwake Simba ndiyo muarobaini
sahihi na utaisaidia klabu hiyo. Nafikiri kuna mengi ya kujifunza
nikianza na yafuatayo.
Mo Dewji:
Mo
Dewji ndiye atakuwa mwekezaji mkuu hapo baadaye kwa kuwa mchakato
umepita na yeye ameshinda zabuni. Hakika ameonyesha mfumo wa
wafanyabiashara walivyo, inapobidi anachukua hatua badala ya kusubiri.
Kuna
haja pia ya kuwa na washauri kwa kuwa ikiendelea hivyo akawa anachukua
uamuzi wake kupitia maumivu ya moyo wake, wakati mwingine haitakuwa
sahihi. Badala yake, linapotokea tatizo vizuri kuangalia mambo kadhaa
kabla ya kuchukua uamuzi.
Viongozi:
Leo
hakuna kiongozi anayewajibika, lakini viongozi wakiwemo wale wa kamati
ya usajili wanajua wapi wamemkwamisha Omog au kumsaidia. Ukweli kuna
sehemu walikuwa na matakwa yao binafsi na tunajua sote ndani ya kamati
kuna wachezaji huletwa na watu na watu wangefurahi kuona waliowaleta
wanacheza.
Kamati
ya Usajili ya Simba si miungu, wao pia wanakosea na hakuna
anayeadhibiwa. Wanaitia klabu hasara na hakuna anayehojiwa, lakini
adhabu ya Omog inaonyesha makosa yao pia na wanahusika.
Kusajiliwa
kwa baadhi ya wachezaji au kuachwa hata kama Omog hakutaka nalo
lilikuwa kosa. Alitoa mapendekezo yake ya mshambuliaji, kipa na beki.
Hayakutekelezwa
yote, amesajiliwa mchezaji asiyemjua, hakupewa hata video, jambo ambalo
kitalaamu nalo si zuri. Mnajua mlimkwamisha wapi, basi vizuri mjipange
ili ajaye msimuangushe na mwisho aadhibiwe yeye.
Wachezaji:
Kama
alivyofanya Mo, nafikiri ingekuwa inawezekana basi Simba ingechukua
hatua kwa wachezaji au kuna haja ya kurekebisha mikataba yao kuwa kama
kuna uzembe kazini adhabu inapita.
Mechi
nyingi za Simba angalia wachezaji walivyo mastaa, ajabu walio Barcelona
na Real Madrid wanajituma kwa juhudi kubwa kuliko walio Simba ambalo ni
jambo la kusikitisha sana.
Simba
iliyoshindwa kuifunga Green Worriers katika dakika 90, wachezaji
wanakwenda kupiga penalti utafikiri mpira ulishaingia wavuni, tena
hawaonyeshi wamelenga kushinda. Wamelegea, hakuna malengo kwenye macho
wala miili yao. Siku ile wachezaji wa Green Worriers ndiyo waliopaswa
kuitwa wachezaji wa Simba na Simba wawe Green Worriers.
Omog
angewaadhibu, uongozi na mashabiki ungepiga kelele. Kwa kuwa wamejenga
mapenzi nao na wamewafanya washindwe kuheshimu anayewaongoza na wanataka
kuheshimu wao juu yake.
Wachezaji wengi wa Simba wanaamini Simba imebahatika “kuchezewa” na wao, hawajui wamekuwa na bahati kubwa kuitumikia Simba!
Mashabiki:
Kundi
la mwisho lenye sapoti kwa timu lakini linaweza kuwa sumu hasa kama
uongozi si imara. Walilia na Mkude arudishwe kucheza wakati kocha
alimuona hana msaada, Mkude alirudi baada ya kushindwa kuonyesha juhudi
akaonyesha baada ya kuona ameombewa nafasi, jiulize awali kwa nini
hakufanya hivyo?
Wachezaji
hawajitambui kwa kuwa wanajua wana watetezi ambao ni mashabiki. Tangu
Mkude amerudi, mara ngapi Simba imetoka sare au imefungwa? Mara ngapi
ameiangusha? Jibu litakuwa “ni mambo ya soka”. Lakini kwa nini kwa Omog
haikuwa “mambo ya soka?”
Kuna
sababu ya kujifunza, mashabiki wajadili na kushangilia kazi wamuachie
kocha na atakayekuja wampe nafasi ili wale waliovimba vichwa awanyooshe
na kazi iwe ya uhakika.
Kila
la kheri Omog, ulistahili kwenda lakini waliokuangusha umewaacha
wanaendelea “kula bata” na sasa watakuwa na muda wa kujituma
kuwasahaulisha Simba kabla ya kuendelea na “kama kawaida” hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment