BAADA
ya hapo jana kupata ushindi katika mchezo wa kombe la Shirikisho la
Azam kwa kuifunga Mufindi United kwa mikwaju ya Penalt mitatu kwa mmoja,
Wanatipilindanda Pamba ya Mwanza wamejipanga kuhakikisha wanasalia
katika ligi daraja la kwanza kwa nguvu zote ,hayo yamesemwa na kocha
mkuu wa timu hiyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa hapo pamba Venance
Kazungu alipokua akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online
‘’Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Mufindi nimewajenga vijana wangu katika hali ya kuapambana na katika hali ya ushindi,kwani nimesajili wachezaji sahihi na katika muda sahihi kama mambo yataenda kama nilivyopanga wakafata kile ambacho tunakifanya mazoezini kwa uvumilivuwao naamini na nauhakika pamba tutabaki ligi daraja la kwanza msimu huu na tupambane kurejea Premier Mwakani baada ya miaka kumi na saba’’
Katika
hatua nyingine Kazungu amewataka wana mwanza kuwa wamoja na kuonesha
uzalendo kwa timu zao tatu zilizoko katika kundi moja la kundi c katika
ligi daraja la kwanza Fdl huku akiomba chama cha soka mkoa wa mwanza
Mzfa kilichoko chini ya Mwenyekiti Vedastus Lufano ambaye ni mjumbe wa
kamati tendaji ya shirikisho la soka Tanzania tff akiwakilisha mikoa ya
Mara na Mwanza kutoiangalia timu moja na badala yake itazame namna gani
watazisaidia timu hizo katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
Ikumbukwe Pamba yenye historia kubwa katika soka la Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la muungano na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa, iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi kumi na mbili nyuma ya Alliance ya Mwanza,Dodoma fc ya Dodoma na Biashara ya Mara na wataanza duru ya mzunguguko wa kumi kwa kusafiri hadi mkoani Mara kuwakabili wenyeji Biashara zamani Police mara kwenye uwanja wa sabasaba wakati Alliance watasafiri hadi Dodoma kucheza Na Dodoma fc katika uwanja wa Mpwapwa ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma michezo yote itachezwa December michezo mingine itakua inazikutanisha Toto Afrika dhidi ya Maafande wa Jkt Orjolo huku Transit Camp wakicheza na Ndugu zao Rhyno Rangers katika uwanja wa Ccm Kambarage mjini Shinyanga michezo yote itachezwa kati ya December thelathini na December thelathini na moja mwaka huu ambapo timu mbili zitapanda ligi kuu Tanzania bara baada ya mizunguko kumi na nne kukamilka
‘’Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Mufindi nimewajenga vijana wangu katika hali ya kuapambana na katika hali ya ushindi,kwani nimesajili wachezaji sahihi na katika muda sahihi kama mambo yataenda kama nilivyopanga wakafata kile ambacho tunakifanya mazoezini kwa uvumilivuwao naamini na nauhakika pamba tutabaki ligi daraja la kwanza msimu huu na tupambane kurejea Premier Mwakani baada ya miaka kumi na saba’’
Kikosi cha Pamba SC kikiwa Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza |
Ikumbukwe Pamba yenye historia kubwa katika soka la Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la muungano na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa, iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi kumi na mbili nyuma ya Alliance ya Mwanza,Dodoma fc ya Dodoma na Biashara ya Mara na wataanza duru ya mzunguguko wa kumi kwa kusafiri hadi mkoani Mara kuwakabili wenyeji Biashara zamani Police mara kwenye uwanja wa sabasaba wakati Alliance watasafiri hadi Dodoma kucheza Na Dodoma fc katika uwanja wa Mpwapwa ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma michezo yote itachezwa December michezo mingine itakua inazikutanisha Toto Afrika dhidi ya Maafande wa Jkt Orjolo huku Transit Camp wakicheza na Ndugu zao Rhyno Rangers katika uwanja wa Ccm Kambarage mjini Shinyanga michezo yote itachezwa kati ya December thelathini na December thelathini na moja mwaka huu ambapo timu mbili zitapanda ligi kuu Tanzania bara baada ya mizunguko kumi na nne kukamilka
No comments:
Post a Comment