Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amezindua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Arusha mjini katika eneo la Njiro Kontena.
Akizungumza
na wananchi ambao wamehudhuria shughuli ya uzinduzi wa hospitali hiyo,
Gambo amesema kwamba anafuraha kushuhudia tukio hili kwani ni moja kati
ya ahadi za Rais Magufuli.
“Nina
furaha sana kushuhudia tukio hili litakaloacha alama katika maisha ya
watu wetu wa Arusha, kwani wakati wa kampeni Mhe Rais Magufuli aliahidi
na tunatekeleza kwa vitendo,” Gambo
Hospitali
hiyo inatarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya laki nne kutoka wilayani
humo na maeneo ya jirani ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanasababisha
hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kuelemewa.
Mhandisi
wa Majengo Jiji la Arusha akitoa maelezo ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) na mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe Fabian
Daqqaro ( katikati).
Aidha
Gambo ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa mapato yanayokusanywa na Jiji
la Arusha kwa mwaka bado hayatoshelezi hata kulipa mishahara ya
watumishi wake na kwa maana hiyo ni muhimu kuweka mifumo thabiti ya
ukusanyaji wa mapato jijini humo.
“Jiji
la Arusha mapato yake ya ndani kwa mwaka hayazidi bilioni 12 na
mishahara pekee ya watumishi wa halmashauri ni zaidi ya bilioni 40, sasa
hapo ukilipa tu mishahara hela yote inakwisha na bado unakua na deni,
sasa hata fedha za maendeleo zitatoka wapi zaidi ya kutegemea hela
zinazoletwa na Magufuli?? Gambo alihoji.
Ujenzi
wa Hospitali ya wilaya ya Arusha kwa awamu ya kwanza unafanyika katika
moja ya maeneo ya wazi yaliyo kuwa yakimilikiwa kinyemelela na baadhi ya
wajanja wachache na kwa sasa ujenzi umeanza ambao utagharimu kiasi cha
shilingi milioni 500 hii ikiwa ni jengo la Ghorofa moja kwa ajili ya
wagonjwa wa nje.
No comments:
Post a Comment