Pages

Sunday, December 24, 2017

“Sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya Simba”-MO Dewji

Club ya wekundu wa Msimbazi Simba Ijumaa ya December 22 2017 ilikuwa katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi kucheza mchezo wake wa round ya pili wa Kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Green Warriors.
Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo, wamekutana na bahati mbaya baada ya kuvuliwa Ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-4, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika game 1-1, goli la Simba likifungwa na John Bocco kwa penati dakika ya 54.

Baada ya Simba kutolewa katika michuano hiyo tumeona reaction za mashabiki lakini mfanyabiashara Mohammed Dewji ambaye ndio mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya Simba ameonesha kukasirishwa kwake na matokeo hayo na kuandika hivi
“Kwa kuwa bado sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya Simba, kama mwanachama na mshabiki wa Simba, namuomba OMOG kwa heshima na taadhima ajiuzulu”>>> MO Dewji
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mfumo wa hisa ukikamilika ndani ya Simba Mo Dewji atakuwa anaimiliki Simba kwa asilimia 49 na wanachama asilimia 51 baada ya December 3 mwaka huu kutangazwa kuwa mshindi wa zabuni kwa Bilioni 20.

No comments:

Post a Comment