Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wanachama wa CCM kuwa
kimepokea taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa kutakuwa
na uchaguzi wa marudio katika Kata na Majimbo yaliyotajwa hapo juu.
Wanachama
wote wenye sifa za msingi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na waliokidhi
vigezo vya uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM na Kanuni zake
wanahamasishwa kujitokeza ili kuomba ridhaa ya Chama kupeperusha bendera
ya CCM katika Uchaguzi huu wa marudio isipokuwa na kama
inakavyoelekezwa na taarifa hii.
Aidha
Chama kimejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na kisayansi, na
zilizosheheni siasa za hoja na zinazojikita katika kushughulika na shida
za wananchi na hatimaye kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huu wa
marudio. Kwa maana hii, msisitizo unawekwa kwa wanao omba ridhaa ya
kugombea, vikao vya uchujaji na mapendekezo, na vikao vya uteuzi
kuzingatia Misingi ya Maadili na kuhakikisha waombaji wana akisi
uaminifu, uadilifu, uchapakazi, heshima kwa watu, ukubalifu wa imani,
siasa na itikadi ya CCM, nidhamu kwa chama na wawe watu ambao umma wa
wananchi unawatambua kwa nafasi yao katika jamii inapokuja katika
kushughulika na shida zao.
KWA WAOMBA DHAMANA YA UDIWANI
Wana
CCM ambao wamejipima na kujitafakari na kuona wanatosha, wanakumbushwa
kwamba kuchukua fomu ya ugombea udiwani katika Ofisi za Kata tajwa hapo
juu ni tarehe 8-11 Januari 2018. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 11
Januari 2018 saa 10:00 jioni. Gharama ya fomu ni Shilingi 10,000/- tu za
Kitanzania.
Wajumbe
wa Mikutano Mikuu ya Kata watapiga kura za maoni tarehe 12 Januari
2018. Kamati za Siasa za Kata zitajadili na kutoa mapendekezo kwa Kamati
za Siasa za Wilaya tarehe 13 Januari 2018.
Kamati
za Siasa za Wilaya zitajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za
Siasa za Mkoa tarehe 14 Januari 2018. Kamati za Siasa za Mikoa
zitajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Mikoa tarehe
16 Januari 2018. Halmashauri Kuu za Mikoa zitajadili na kufanya uteuzi
wa mwisho tarehe 17 Januari 2018
Wagombea
walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushiriki katika uchaguzi wa
Udiwani katika Kata nne watachukua fomu kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi
ngazi ya Kata katika kata husika tarehe 18-19 Januari 2018 na zoezi
hili litafanyika chini ya usimamizi wa Katibu wa CCM wa Wilaya.
UCHAGUZI WA MARUDIO KWA MAJIMBO YA SIHA NA KINONDONI
Baada
ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwa mamlaka iliyokasimiwa
kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Ndg. Dkt.
Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na
Ndg. Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar
es Salaam.
Aidha
wagombea wa Ubunge wanaelekezwa kufika katika Ofisi za Chama Cha
Mapinduzi (CCM) katika Mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo
Uchaguzi kutoka kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa hiyo siku ya Jumanne,
tarehe 9 Januari 2018 bila kukosa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
06 Januari 2018
No comments:
Post a Comment