Serikali
kupitia Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) imetangaza mchakato wa awali wa
zabuni ya ununuzi wa vichwa na mabehewa kwa ajili ya treni ya umeme
itakayotumika katika reli ya kisasa (Standard Gauge) ambayo ujenzi wake
unaendelea.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia Idara ya
Habari (MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata taratibu za
kimataifa za ununuzi kwa njia ya ushindani.
Kwa
mujibu wa tangazo la zabuni, jumla ya vichwa 14 vya treni ya umeme kwa
ajili ya kusafirisha mizigo na vichwa viwili vya treni ya mizigo
inayotumia mafuta vinahitajika.
Aidha,
RAHCO pia imetoa zabuni ya ununuzi wa vichwa vitano vya treni ya abiria
ya kisasa inayotumia umeme (Electric Multiple Units) ambapo kila kimoja
kitakuwa na uwezo wa kuvuta mabehewa 60 yenye kuchukua abiria 1,800.
Katika mabehewa hayo ya abiria, mabehewa 15 yatakuwa ni ya kiwango cha daraja la kwanza na mengine 45 ni daraja la pili.
Mbali
na mabehewa ya abiria, zabuni hiyo inajumuisha ununuzi wa mabehewa
mengine zaidi ya 1,500 yenye muundo tofauti kwa ajili ya kubebea aina
mbalimbali za mizigo.
Pamoja
na sifa mbalimbali zilizo ainishwa katika tangazo la zabuni, moja ya
sifa za reli hiyo ya kisasa ni kuhimili treni ya abiria yenye uwezo wa
mwendo kasi wa kilometa 160 na mabaehewa yenye juma ya urefu wa mita
2000, wakati ile ya mizigo yenye uwezo wa kwenda kasi ya kilometa 120
kwa saa.
Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, mwisho wa kuwasilisha nyaraka za zabuni ni Januari 30, mwaka huu.
Tayari
awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hii kutoka Dar es Salaam mpaka
Morogoro inaendelea na wakati huo huo tayari Serikali imesaini mkataba
kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi kutoka Morogoro hadi Makutupola
mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment