Pages

Saturday, January 6, 2018

Kauli ya CUF baada ya CCM kumteua Mtulia kuwa mgombea Ubunge Kinondoni

Waheshimiwa Watanzania, tumepigiwa simu na Wanahabari kutaka kujua msimamo wa CUF kuhusu uteuzi uliofanywa na CCM dhidi ya Maulidi Saidi Mtulia kugombea Jimbo la Kinondoni. 
Kwanza tunapenda Watanzania watambue kua Mtulia si Mwanachama wa CUF na katika hali hiyo, Cuf hawezi kua na sababu yoyote ya kushangazwa na uteuzi huo.

Pili Watanzania wanapaswa kutambua kwamba CCM kama Chama wanayohaki ya kumsimamisha Mtulia kua ni Mgombea wao japo Uamuzi huo unaweza kua na mtimanyongo kwa wanaccm na hata wasiokua wanaccm kutokana na tamaduni za CCM au historia ya Mtulia mwenyewe kwakua kabla hajajiuzulu alishakua Mbunge.

CUF – Chama cha Wananchi kinamtazama Mtulia kama CHAMBO KWENYE NDOANO YA KUVULIA SAMAKI, Mtulia ni kivutio cha Utalii, ili Mbuga ya Wanyama itembelewe na Watalii wengi lazima pawepo na kivutio. 
Uteuzi wa Mtulia utawavuta wengi kwenye CCM wakiwa na Mategemeo kua na wao wakifanya kama alichofanya Mtulia basi watateuliwa kua Wagombea kwenye Majimbo yao ya awali. 
Lakini Chambo kwenye NDOANO ni ngumu kumpata ila anarahisisha kuvuliwa au kupatikana kwa Samaki wengi. CUF – Chama cha Wananchi kitawashinda Wagombea wa Vyama vingine wataoshiriki kwenye Uchaguzi huo. Tumeshaanza maandalizi muda mrefu na tuna Mgombea mzuri, tuna uhakika wa kushinda kwenye Jimbo hilo la Kinondoni.

Wito wetu kwa Watanzania wajitokeze Kwa wingi kupiga Kura za kukataa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma yanayofanywa na Maulidi Mtulia kwa kutuingiza kwenye Uchaguzi usiokua wa lazima na CCM nayo kuridhia Matumizi hayo kwa kurejesha jina la Mtulia kugombea nafasi ambayo alikua nayo hapo awali. Haya ni matumizi mabaya yalioridhiwa na CCM kwa kumrejesha Mtulia kama Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM.

Watanzania bado tunachangamoto nyingi katika sekta mbali mbali kama vile Elimu, Afya na Miundombinu duni ndani ya Nchi yetu ambapo Fedha hizi za Uchaguzi zingeweza kuelekezwa huko. Kataaeni Matumizi haya kwa kushiriki kikamilifu kwenye Marejeo ya Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mwezi February

No comments:

Post a Comment