Salaam za mwaka mpya toka kwa Haji S Manara.
Msemaji wa Simba SC
Awali ya yote tumshukuru sana Mungu mwenyezi kwa kutuwezesha sote kuumaliza mwaka 2017 na kuuingia mwaka huu mpya wa 2018.
Mwaka tulioumaliza ulikuwa na changamoto nyingi sana kama ilivyo kwa miaka yote ya nyuma.
Changamoto tulizopitia ni za kawaida sana ingawa nyingine zilikuwa ngumu sana, kiasi cha kwamba zimeacha doa kwenye maisha yetu.
Mojawapo ya changamoto iliyonigusa sana mwaka jana, ni kushtakiwa kwa viongozi wakuu wa klabu nnayoisemea ya Simba.
Kufunguliwa
kwa Shauri lile sio tu kulinihuzunisha, bali kulinifanya niwe muoga
sana kwa kila kitu. ila kama nilivyoandika ni changamoto tu na mwanadamu
huna budi kupitia mitihani ya aina hii ili kukamilisha ubinadamu wako,
sote tumuombe Mungu aiwezeshe kesi hii iishe haraka na haki ipatikane
kwa pande zote.
Mwaka
jana pia kama klabu na kama Timu tulipata changamoto kubwa ya vyombo
vyenye maamuzi ya kuongoza Soka nchini, kutoitendea haki klabu yetu kwa
mambo kadha wa kadha, sio nia yangu kufukua makaburi, lakini lazma
tujikumbushe ile kadhia tata ya kadi tatu za njano, ambayo kwa maksudi
kabisa waliokuwa viongozi wa TFF waliamua kulipindisha jambo lile ili tu
waliepanga awe bingwa kupata walichopanga.
Haiwezekani
na ntaendelea kuamini kamati iliyofanya maamuzi ya kuipoka Simba points
tatu, haikuwa na mamlaka yoyote ya kutolea maamuzi ya jambo liliotokea
uwanjani, Sote tunajua kila shauri hutolewa uamuzi na chombo 'Makhsuus'.
Itakuwa
ajabu ya karne eti Mahakama ya Ardhi kutolea maamuzi kesi za ubakaji,
au kamati ya Bunge ya maadili kutolea uamuzi kesi za Trafik, ni kituko
kikubwa kuwahi kutokea nchini.... kwangu ulikuwa uonevu mkubwa zaidi
kuwahi kutokea nchini, Lakini yalishaisha na sisi kama klabu tuliamua
kusonga mbele zaidi.
Ni
kweli Simba iliamua kulalamika FIFA baada ya kuona hatutapata haki kwa
TFF ile, lakini chombo hicho kikubwa zaid duniani kilitujibu kwa njia ya
DHL,ya kwamba tutumie vyombo vya ndani kwenye Shirikisho na ushauri wao
kwetu pia ulilenga kuzingatia muda wa malalamiko yetu.
Busara
ya uongozi wa Simba chini ya kaimu Rais wa Simba Salum Abdallah kwenye
jambo hili ilikuwa kubwa sana, kwa kuwa majibu ya FIFA yalichelewa na
teyari uongozi mpya wa TFF ulishaingia madarakani, na kwa kuwa hata
waliobebwa wanajua kuwa walibebwa na kwa kuwa hatukutaka kuwapa msuguano
na wadau wake TFF mpya, ukizingatia walifungua ukurasa mpya kwenye Soka
nchini, Simba iliamua kuachana na rufaa ili ijikite kwenye msimu huu
tulionao sasa.
Ifahamike
pia kombe la Ubingwa wa msimu uliopita lilikabidhiwa haraka haraka ili
kutoa ugumu kwa haki sio kutendeka bali kuonekana imetendeka.
Nyote
mnafahamu kitendo cha dhulma ile ilinipelekea mm kufungiwa mwaka mmoja
na faini ya Shilingi milioni tisa, Lakini nishukuru kamati ya Nidhamu ya
TFF na uongozi wa Shirikisho kwa kuniondolea adhabu ile iliyotolewa
bila kunipa haki ya kusikilizwa (Natural justice).
Kwa
kweli kipimo cha uonevu msimu uliopita kinahitaji kiwekwe kwenye
maandishi ya 'Riwaya' itakayosomwa na vizazi vingi vijavyo..Ila kwa
kadri nijuavyo uongozi wa klabu, mm mwenyewe na wanasimba wote
wamesamehe, tusonge mbele, yaliyopita c ndwele tugange yajayo.
Mwaka
jana klabuni pia tulianza mchakato mkubwa wa kuingia kwenye mabadiliko
ya kimuundo na kimfumo ya klabu yetu. Mchakato huu ulienda vzuri sana na
tupo kwenye hatua za mwisho mwisho kuwezesha klabu kuanza rasmi
kuutumia muundo huo wa hisa.
Muundo
huu utaiwezezha klabu yetu kuwa klabu tajiri miongoni mwa vilabu tajiri
Africa, Utajiri huu tunaamini utaiwezesha klabu kuwa na uwezo mkubwa wa
kujiendesha na kuwa rasimali zitakazotuwezesha kuwa na mafanikio ya
ndani na nje ya Uwanja.
Kwenye
mchakato huu pia tulipata changamoto mbalimbali. lakini Alhamdulillah
kwa sehemu kubwa tumevuka salama. na kwa sasa milango ipo wazi kwa wale
waliotaka kukwamisha kujirudi na sote kwa pamoja tuje tujenge Klabu
yetu..ukizingatia tuna kauli mbiu isemayo SIMBA NGUVU MOJA
Kwenye
changamoto hakukosi mafanikio. licha ya kukoseshwa ubingwa kwa figisu
figisu.Simba ilifanikiwa kushinda kikombe cha Shirikisho ambacho
kimetuwezesha kupata nafasi ya kuwakilisha nchi mwaka huu kwenye
michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika(Caf).
Msimu
huu uongozi wenu umejitahidi kuwasajili wachezaji bora zaid ambao sio
tu waturejeshee ubingwa wa ligi, bali kufanya vema kwenye michuano hyo
ya Afrika.
Kwa
sasa bado tunaongoza ligi kuu na wachezaji wetu hawadai shilingi ya
mishahara, na wanajua kiu ya wanasimba msimu huu.. pia uongozi unatambua
changamoto tuliyokutana nayo msimu uliopita, wale wanaodhani msimu huu
kutakuwa na yale yale ya msimu uliopita tuwaambie wasubiri, Sababu
hatuamini TFF hii inae bingwa iliempanga na hakutakuwa na uchakachuaji
wa ratiba na waamuzi. basi InshaAllah bingwa halali atapatikana msimu
huu.. na kwa maandalizi tuliyoyafanya na kwa matakwa ya Mungu Simba
itachukua ubingwa safari hii.. hilo ndio lengo letu na dhamira ya klabu.
kubwa tunawaomba wanasimba tudumishe umoja na mshikamano wetu.
tuvumiliane, tukosoane kistaraabu, tusitoe fursa kwa wapinzani wetu na
kwa wachezaji watambue kile alichokisema Bwana MO pale Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere.. thamani ya kuvaa jezi ya Simba, thamani ya kuichezea Simba,
sote tutambue sisi ndio klabu kubwa nchini, klabu ya watu, klabu maarufu
zaid ndani na nje ya nchi. na tujue nn tunataka msimu huu na mwaka huu
kwa ujumla.
Mwisho
niwaombe
sote tuendelee kuwaombea viongozi wetu wa nchi. wale wa Serikali
wakiongozwa na Rais wetu Mh John Magufuli. wale wa vyama vya siasa, na
wale wa taasisi zingine, hikima,busara,kumjua Mungu,upendo na uzalendo
na kwa viongozi wa TFF tuwaombee waendelee kutenda haki.
Asionewe mtu wala asipendelewe mtu. klabu zote ziwe sawa.
Ratiba iwe rafiki kwa klabu zote.
Waamuzi
wachezeshe kwa haki mechi zote, tunajua mapungufu ya kibinadaam yapo
ila mapungufu hayo yasiwe yanawapa upendeleo timu moja tu.
Sote tukiamua tunaweza kwa maslah mapana ya mchezo wa Soka nchini.
Kwa niaba ya Uongozi mzima wa klabu. benchi la ufundi. wachezaji, wanachama, washabiki wote wa Simba niwaambie
Happy New year 2018
IMETOLEWA NA....
HAJI S MANARA
Mkui wa Habari Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA
No comments:
Post a Comment