Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amekubali kuwa timu yake ilizidiwa na Mbao na kujikuta ikiruhusu magoli mawili ndani ya kipindi cha pili, mlinzi huyo wa zamani wa kulia wa Yanga na Taifa Stars amesema kipindi cha pili Mbao walibadilika na kutumia nafasi walizozitengeneza kupata magoli.
Nsajigwa amekubali kuwa Mbao walistahili kushinda mchezo huo baada ya kufanya kazi yao vizuri uwanjani.
“Hali ya mchezo kwa ujumla ilikuwa nzuri kiasi chake, kipindi cha kwanza mechi ilikuwa nusu kwa nusu lakini kipindi cha pili kilibadilika, Mbao walibadilika wakaja juu badae wakapata nafasi wakazitumia. Mpira ni mchezo wa matokeo, usipobadili nafasi ulizopata kuwa magoli basi huezi kufunga”-Shadrack Nsanjgwa.
“Tumepoteza mchezo tunawapa hongera Mbao wamefanya kazi yao vizuri wamepata ushindi.”
Nsajigwa akishirikiana na benchi la ufundi la Yanga alikiongoza kikosi kwenye mchezo dhidi ya Mbao bila uwepo wa kocha mkuu George Lwandamina ambaye yupo kwao (Zambia) ambako amekwenda kuhudhuria msiba wa mtoto wake aliyefariki hivi karibuni
No comments:
Post a Comment