Katika
hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani
Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya
nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji
utokanao na unga wa muhogo.
Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.
Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji huo.

No comments:
Post a Comment