Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa neno kwa mara ya kwanza kwa
mwaka 2018 kuhusu ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q400 iliyozuliwa
nchini Canada na Meli ya iliyosajiliwa kwa namba za Tanzania
iliyokamatwa huko Jamhuri ya Domica na Shehena ya dawa za kulevya.
Kuhusu
Bombardier Serikali kupitia kwa Msemaji wake Mkuu, Dkt. Abbas Hassan
amesema bado ratiba ipo vile vile kuwa ndege hiyo ya Bombardier na ile
kubwa ya Dreamliner zote zitafika nchini kati ya mwezi Juni na Julai
mwaka huu.
“Ishu
ya ndege tutaizungumza itakapofika wakati wake lakini mara ya mwisho
nilisema ndege zote za serikali ambazo tumenunua ratiba yake ni kufikia
mwezi Juni- Julai mwaka huu ndege zote nne ikiwemo ile ndege ya ndoto
yetu ya Boeing Dreamliner zitakuwa zimefika nchini.“amesema Msemaji Mkuu
wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwenye mkutano wake na Waandishi wa
Habari.
Kwa
upande mwingine Serikali imekiri kupokea taarifa za Meli yenye usajili
wa Tanzania kukamatwa kwenye visiwa vya Jamhuri ya Dominika ikiwa na
shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine.
“Suala
la meli iliyokamatwa Dominika hili nalifahamu, nimelisikia kwa hiyo
wenzetu wa wizara ya mambo ya nje bado wanafuatilia kujua usahihi
maanake imeripotiwa hivyo kwa hiyo wizara ya nje tumeshazungumza nao na
wanalifanyia kazi kwahiyo kama kutakuwa na taarifa zitatolewa.“amesema
Dkt. Hassan Abbasi.
Mnamo
Desemba 31, 2017 Jeshi la Maji nchini Uholanzi liliikamata Meli yenye
usajili wa Tanzania ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine
tani 1.6 ambapo Meli hiyo pamoja na wahusika waliokuwemo walishikiliwa
nchini Jamhuri ya Dominika kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment