Pages

Sunday, December 24, 2017

ACHANANA MATOLA, SIMBA IMEANZA MAZUNGUMZO NA KOPUNOVIC




Pamoja na kuwepo kwa taarifa kwamba Simba imeanza kumuwania Selemani Matola ili kukinoa kikosi chake akisaidiana na Masoud Djuma, taarifa za uhakika zimeeleza, Simba imefanya mazungumzo na Goran Kopunovic.

Kopunovic alikuwa Simba kabla ya kuamua kuondoka baada ya dau alilotaka kulipwa kushindikana.

Kocha huyo aliiwezesha Simba kubeba Kombe la Mapinduzi mara tu baada ya kujiunga nayo.

Simba imeanza mazungumzo na kocha huyo baada ya kumuondoa Joseph Omog ambaye atarejea kwao Cameroon.


Uongozi wa Simba umeingia kwenye hasira baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na kikosi cha daraja la pili cha Green Worries.

No comments:

Post a Comment