Pages

Monday, December 25, 2017

CANNAVARO AAMUA KUFUNGUKA KUHUSIANA NA ISHU YAKE YA KUSTAAFU


Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannnavaro’, amenyoosha mikono juu na kutamka kuwa inatosha na sasa ataitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja pekee.
Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya timu hiyo kumsajili beki wa kati Mkongo, Fistoni Kayembe kwa mkataba wa miaka miwili.

Cannavaro anapambania nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mabeki wanne ambao ni Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Mkongo huyo.



Cannavaro alisema anaamini muda wake wa kucheza umefikia kikomo, hivyo ni wakati wa kustaafu kucheza kwa ajili ya kuwaachia vijana wengine wanaochipukia kuonekana.
Cannavaro alisema, akiwa anaendelea kuitumikia Yanga, anasubiria kozi ya makocha ya hatua ya awali ianze ili na yeye aanze mafunzo kwa ajili ya maisha yake ya badaye.

Aliongeza kuwa, amepanga kufanya kazi hiyo ya ukocha kutokana na maisha yake yote kuhusisha soka, hivyo hataki kutoka nje ya soka zaidi ya kujiongezea elimu.

“Kiukweli muda wangu wa kuendelea kuichezea Yanga umebaki mdogo na nilichopanga ni kuitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee.


“Mara baada ya kuachana kuichezea Yanga, basi ndiyo itakuwa mwisho wangu wa kucheza soka na badala yake nitastaafu kabisa na kuingia kwenye kazi ya ukocha,” alisema Cannavaro.

No comments:

Post a Comment