Pages

Thursday, December 28, 2017

Waziri Mkuu awataka vijana kuchangamkia fursa




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi huku akiwataka vijana kuchangamkia fursa kwa kuandaa mitaji ya kuwa na gereji za kuchomelea vyuma.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi katika vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho, alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na ku,uagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.
“Nilileta makontena yenye vifaa vya hospitali, na humo ndani mlikuwa na vifaa vya kuwatunza watoto njiti (watoto wanaozaliwa kabla ya muda kutimia). Hakikisha hawa wanapata kifaa hicho kwa sababu hawana gari la kubeba wagonjwa, na pia wako mbali na hospitali ya wilaya na pia kituo cha afya cha jirani kiko mbali pia,” alisisitiza.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-Mibure.”
Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa k, saluni na viwanda vidogo vya usindikaji.
Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Mibure mbele ya Waziri Mkuu, Mwenyeiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Chilemba alisema mradi huo umekwishagharimu sh. milioni 52, ambapo kazi zilizokamilika ni jengo la zahanati, kichomea taka na choo chenye matundu matatu.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kupanda holela kwa gharama za vifaa vya ujenzi, kupokea michango kidogo kutoka kwa wananchi, ukosefu wa nyumba ya mganga na wauguzi na kiasi cha fedha cha sh. milioni 8.26 za kununulia samani.
Bw. Chilemba alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia wakazi wa vijiji jirani vya Njawale, Namakuku, na vijiji jirani vya wilaya ya Nachingwea ambavyo vinapakana na wilaya ya Ruangwa.

No comments:

Post a Comment