Pages

Monday, January 1, 2018

Zitto Kabwe ametaja lengo la waliotaka kumuua Tundu Lissu

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameuzungumzia mwaka 2017 huku akiukaribisha mwaka mpya 2018, kwa kusema kuwa tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilimgharimu.

==>Hapo chini ni ujumbe wa Zitto Kabwe
Tunawatakia heri ya mwaka mpya 2018. Mwaka 2017 ulikuwa na changamoto lukuki lakini pia mafanikio makubwa kwetu kama chama. Mkutano wa miaka 50 ya Azimio la Arusha jijini Arusha ilikuwa mafanikio ya juu kiitikadi. Kwangu Mimi Hotuba ya Arusha ilikuwa bora kimaudhui na ilipaswa tutoe kitabu cha Hotuba ile.

Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Jijini Mwanza kuhusu Maendeleo bila kupoka Uhuru wa watu ulitusaidia kuweka msimamo wetu kuhusu ubinywaji wa haki na Uhuru unaoendelea nchini.

Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile. Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi.

Kuondoka wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa Sana na hivyo Tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018.

Chama chetu kinawatakia heri ya mwaka 2018. Tunamshukuru Mungu kwa mwaka 2017

No comments:

Post a Comment