Pages

Tuesday, December 26, 2017

Kiongozi anayepinga utawala wa Rais Putin azuiliwa kugombea urais nchini Urusi

Kiongozi mkubwa wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny amezuliwa na Tume ya Uchaguzi kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Alexei Navalny
Tume kuu ya uchaguzi nchi humo imesema kuwa Navalny hataweza kugombea kwa sababu alipatikana na tuhuma za ufisadi.
Hata hivyo, Bw. Navalny (41) kupitia ukurasa wake wa Twitter ameshinikiza vyama vingine vya upinzani nchini humo kususia uchaguzi mkuu unaofanyika mwakani mwezi Machi huku akiwataka wananchi waandamane kupinga hatua iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi nchini humo.
Navalny ndiye kiongozi pekee wa upinzani nchini Urusi aliyetajwa kuwa na nguvu ya kupambana na Rais Putin kwenye uchaguzi ujao.
Umaarufu wake ameupata kutokana na kampeni ya kupinga ufisadi na maanadamano dhidi ya Bw. Putin, Bw Navalny alihukumua kifungo cha nje cha miaka mitano mapema mwaka huu kwa mashtaka yanayohusu matumizi mabaya ya fedha.

No comments:

Post a Comment