Siku
moja baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Juliana Shonza kumtaka msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’, kuripoti
ofisini kwake, msanii huyo ameamua kwenda Baraza la Sanaa Tanzania(
Basata).
Gigy
ambaye alijipatia umaarufu kutokana na kupiga picha za kutatanisha na
kuzirusha katika mitandao mbalimbali ya kijamii, amesema ameamua kwenda
Basata baada ya kuambiwa waziri hayupo.
Hata
hivyo, amesema mpaka sasa hajui kosa analoitiwa na kama ni picha za
utupu mbona ameshaacha tabia hiyo siku nyingi na sasa yupo busy kulea
mimba yake.
“Najua
wapo watu wanaodhani naitwa kwa ajili ya tabia zangu za kupiga picha za
utupu, lakini mimi hayo mambo nishayaacha muda mrefu nadhani kwa
wanaonijua Gigy wa sasa hivi sio wa kipindi kile, ila ngoja nisubiri
waziri atakachoniambia japo najiona sina kosa lolote nililotenda kwa
sasa tangu Rais alipotoa onyo kwa wasanii wanaovaa vibaya.
“Pia
kwa wale wanaodhani labda ni kutokana na wimbo wangu wa Papa, binafsi
sina wasiwasi nayo kwa kuwa mimi nilimaanisha samaki, sasa kama kuna
watu wameitafsiri kivingine ni wao,” amesema .
Kwa
upande wake Katibu wa Basata, Godfrey Mngereza alikiri msanii huyo
kufika katika ofisi zao zilizopo Ilala leo na kueleza kwamba hilo
halimuondolei kuitikia wito wa waziri kwa kuwa yeye ndiye aliyemuita.
Mngereza
amesema alichokiona kwa msanii huyo ni kwenda kwao akijua kwamba baraza
hilo ndio mlezi wa wasanii na kubainisha kuwa hata wao walikuwa
hawafurahishwi na aliyokuwa anayafanya msanii huyo japo hawajawahi
kumuita hata siku moja.
No comments:
Post a Comment