Baada
ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kumtembelea Rais
John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo,
Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe amesema kuwa kile kilichosemwa
na Lowassa sio msimamo wa CHADEMA bali ni mawazo yake binafsi.
Akizungumza
jana na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji BBC, Mbowe alisema
wao kama Chama wamekuwa na utaratibu wa kutoa msimamo wao na kueleza
kuwa kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na malalamiko dhidi ya Rais na
Serikali yake kuhusu kuminywa kwa Uhuru wa Bunge, Mahakama na kuminya
Demokrasia.
"
Tunaona jinsi ambavyo uhuru wa watu unaminywa, uhuru wa vyombo vya
habari, wandishi, wanasiasa na wananchi kutekwa, kudorora kwa uchumi,
unaanzaje kumuunga mkono Rais nafikiri muhusika aulizwe mwenyewe," alisema Mbowe.
Kuhusu
kauli ya Lowassa kusifia ongezeko la ajira, Mbowe anasema hayupo tayari
kujibu hoja hiyo lakini akaeleza namna ambavyo makampuni mengi
yanafungwa hivi sasa, kundi kubwa la vijana wasio na ajira likiwa
mitaani.
"
Nisikitike tu kuwa sisi tuna tatizo kubwa sana la kumuuguza Lissu
ambaye alipigwa na risasi, kweli anaweza kutoka kiongozi mkubwa na
kumsifia Magufuli wakati tunauguza watu?
"Msaidizi
wangu Ben Saanane amepotea hadi leo, wabunge wetu wanafukuzwa bungeni
hivyo niseme tu hakuna msimamo kama huo ndani ya Chama labda atafutwe
muhusika mwenyewe aeleze," Alisema Mbowe.
Akizungumzia
hama hama kwa wabunge na wanachama wa upinzani na kujiunga na CCM
sambamba na tukio la jana la Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho,
Muslim Hassanal kujiunga na CCM , Mbowe alisema suala la wapinzani
kuhamia CCM halijaanza leo na kwamba suala la kujenga upinzani ulio
imara lazima lipitie hatua mbalimbali ili kufanya mchujo wa kubakia na
watu wenye dhamira ya kweli.
No comments:
Post a Comment