Baada
ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu
Leo January 9, 2018 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yupo
nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ametoa mtazamo wake kuhusu suala
hilo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu amepost picha inayomuonesha Lowassa akiwa Ikulu na kuandika maelezo haya; “Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu.”
“Lakini
ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na
washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima
viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote
tuwe kwenye ukurasa mmoja.
“Viongozi
na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa
risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye. Katika mazingira ya kesi
nyingi za kutunga dhidi yetu, ‘kazi nzuri’ inayofanywa ina maana gani,
kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.
“Katika
mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa
Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba ‘anafanya kazi nzuri’ ni ‘kumtupia
taulo’ la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia
Watanzania katika miaka hii miwili.
“Kwa vyovyote vile, kitendo cha Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.”– Lissu
No comments:
Post a Comment