Baada
ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kumuita msanii wa Bongo Fleva Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa
mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zinaonekana zipo kinyume na
maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa, Hatimaye Mchekeshaji maarufu
nchini Tanzania, MC Pilipili ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na
kuishauri iendelee kuwasaka wengine wanaofanya hivyo.
MC
Pilipili amesema amepokea taarifa hizo kwa mikono miwili ingawaje
amesema kuna watu wengi mitandaoni wanafanya makosa kama hayo ya kuvaa
nguo fupi au kuonesha maungo yao kwenye mitandao.
“Hiyo
hatua mimi nimeipenda kwanza imeturudisha kwenye Maadili..Unajua hapa
Bongo mtu anaweza akawa maarufu kwa kuposti maumbo yake tuu mtandaoni
hii ni kinyume cha maadili,“amesema MC Pilipili na kuwataja watu wengine
wanaokaa uchi mitandaoni
“Nilipatwa
na maswali juzi Sancho ameitwa, Gigy Money kaitwa lakini pia kuna
msanii mwingine alikuwa maarufu kwa kuposti picha kama hizo amejichora
mitatuu anaitwa Agness, mwingine anaitwa Kim Sasha lakini wakati huo
namuona Idris naye amevaa chupi hivi ile haihamasishi au naye
aitwe?“amesema MC Pilipili.
No comments:
Post a Comment