Tanzania
inataraji kuwa wenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa.
Mkutano
huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad Ahmad, Makamu wa
Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa FIFA na CAF
ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018
Ajenda
za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani
ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward
Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda
nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya
Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake
Nchi
zitakazoshiriki ni Bahrain,Palestina,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za
Kiarabu(UAE),Algeria,Burundi,Africa ya Kati,Ivory
Coast,Mali,Morocco,Niger,Tunisia,Bermuda,Monserrat,St,Lucia,Us
Virgin,Maldives,Congo na wenyeji Tanzania.
Akizungumzia
Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania Rais wa TFF Ndugu
Wallace Karia alisema TFF inajivunia kupata uwenyeji huo mkubwa wa
mkutano wa FIFA na hiyo inachangiwa na mahusiano mazuri na wadau
mbalimbali ambayo yamezaa matunda.
Rais
Karia ameongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa Serikali kupitia Wizara
zake kuweza kutumia fursa hiyo ambayo inaweza kusaidia katika upande wa
Uchumi.
No comments:
Post a Comment