Raisi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia
amesema yeyote atakayebainika kufanya vitendo visivyo vya kiungwana
kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza inayoendelea TFF haitasita
kuwachukulia hatua.
Rais
Karia alisema yapo malalamiko ambayo yanafanyiwa kazi yanayohusu
michezo iliyohusisha Dodoma Fc vs Alliance na Biashara Mara vs Pamba ya
Mwanza ambapo utaratibu utafuatwa na yeyote atakayebainika hatua dhidi
yake zitachukuliwa.
Ameongeza
kuwa tayari amemuagiza Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred kukutana
na kamati ya Waamuzi ambao ndio wenye jukumu la masuala yote yanayohusu
waamuzi ili kuangalia kama Waamuzi wanaotumika wana uwezo wa kuchezesha
kwa kiasi gani.
Aidha
Rais Karia amesema TFF inashirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa nchini (TAKUKURU) ili kudhibiti vitendo visivyo vya kiungwana
na Taasisi hiyo itapatiwa ratiba ya mechi zote ili iweze kufuatilia kwa
ukaribu.
Vilevile
amesema TFF na Bodi ya Ligi wanashirikiana kwa karibu kuhakikisha
anayeshinda ashinde kihalali kwa uwezo akitolea mfano namna mashindano
ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa namna yanavyochezeshwa kwa
haki na kuleta mvuto.
Amesema ni wakati wa kushirikiana kwa kila mmoja ili mpira uchezwe na kuondoa malalamiko ya kila wakati.
No comments:
Post a Comment