Kufuatia
barabara, madaraja na mitaro kujaa maji jijini Dar es Salaam kutokana
na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, kampuni
inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart)
imesitisha kwa muda huduma za mabasi yake.
Taarifa
iliyotolewa leo Jumatatu Januari 8 Mkuu wa mitengo cha mawasiliano wa
kampuni hiyo, Deus Bugaywa imesema huduma hizo zitarejea mara baada ya
hali kutengamaa.
“Kutokana
na maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi kwenye barabara ya
Morogoro na kusababishwa kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo, kampuni
ina uarifu umma kuwa huduma za mabasi hayo zimesitishwa kwa muda,”
imesema taarifa hiyo na kuongeza,
“Imesitishwa
kuanzia saa 3:00 asubuhi, mara baada ya hali kutengemaa na mamlaka
husika kuruhusu barabara hiyo kuendelea kutumika, huduma zitarejea mara
moja.”
No comments:
Post a Comment