Siku
chache tu baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii sauti
iliyodhaniwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka
akijadili namna ya utendaji wa Bunge na Awamu ya Tano ya Rais Magufuli
mwenyewe ametolea ufafanuzi.
Akizungumza leo Jumatano Januari 10, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Longido, Sendeka amesema taarifa hiyo iliyoanza kusambaa tangu juzi inapaswa kupuuzwa.
Akizungumza leo Jumatano Januari 10, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Longido, Sendeka amesema taarifa hiyo iliyoanza kusambaa tangu juzi inapaswa kupuuzwa.
Ameeleza
kuwa sauti hiyo siyo ya kwake na kwamba imetengenezwa na kuongeza
kwamba sauti hiyo imetengenezwa na wapinzani ili kumfarakanisha yeye na
viongozi wa serikali na walio chini yao.
“…
umahiri na heshima niliyoipata nchini na kwenye Bunge ni kubwa.
Nilikwenda bungeni kutimiza wajibu kama mtuhumishi makini, sikwenda
bungeni kuongeza idadi ya wabunge, nilikuwa mwakilishi nyinyi mnajua na
Tanzania inajua"alisema.
Amesema vyama vya upinzani vimepata kiwewe na kuanza kumgombanisha na viongozi wa Serikali kwa kusambaza habari za uongo.
Amesema vyama vya upinzani vimepata kiwewe na kuanza kumgombanisha na viongozi wa Serikali kwa kusambaza habari za uongo.
“Naomba
mzipuuze habari hizi kwa kiwango kinachostahili kwani zote ni uzushi
mtupu , badala yake elekezeni macho, fikra na mikakati yenu katika
uchaguzi unaokuja.” Amesema RC Ole Sendeka.
Tayari
Bunge kupitia kwa Spika Job Ndugai limemwandikia barua Ole Sendeka ili
akahojiwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na
kauli hiyo.
No comments:
Post a Comment