Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya uwepo wa vipindi
vya mvua kubwa inayozidi milimita 50, katika baadhi ya mikoa hapa
nchini.
Katika
taarifa iliyotolewa leo na TMA, maeneo yaliyotahadharishwa juu ya uwepo
wa vipindi vya mvua kubwa ni maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja
na maeneo ya Morogoro kusini.
Mamlaka
imeeleza kuwa hali hii inatokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa
mvua (Inter Tropical Convegence Zone – ITCZ) na mgandamizo mdogo wa hewa
ulioko kwenye mkondo wa bahari wa Msumiji.
TMA
imezitaka mamlaka husika, wadau wa mazingira pamoja na wakazi wa maeneo
husika kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa
zinazotolewa, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua
hiyo.
No comments:
Post a Comment