Rais
Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa
katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo
Ijumaa Januari 12, 2018.
Magufuli
ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka
Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amemuelekeza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa
endapo mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika
waachie ngazi.
“Wakulima
wanataka mbolea na muda ni huu, inasikitisha sana, fedha kwenye bajeti
zimetengwa lakini mpaka leo mbolea haijawafikia wakulima, sasa mkoa kama
Rukwa ndio tunaoutegemea kwa chakula, waziri yupo na watendaji wake
wapo lakini mpaka leo mbolea haijapelekwa, wakulima watazalishaje
chakula?
Rais
Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao
ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote
atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.
“Nataka
kila mmoja afanye kazi, Watanzania wanataka maendeleo, hakuna muda wa
kubembelezana, kila mmoja afanyie kazi mambo yanayomhusu asisubiri
kuambiwa, kule bandarini niliunda timu za kuchunguza madudu yaliyopo
huko naambiwa kuna makontena 178 ya makinikia hayana mwenyewe, mengine
yapo Ubungo, mengine bandari” ameongeza Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment