Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini.
Rais
ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa
hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa
Naibu Waziri wa Madini.
“Nimesikia
tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa
madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye
mtendaji na msimamizi mkuu wa madini.
“Mambo
ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume
kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi.
Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo
makontena bandarini na pale Ubungo.
“Mimi
sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata
wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za
sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi,
tafuta watu wa kukusaidia na mkamalize hayo,” alisema Magufuli.
Kamishna
aliyekuwepo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amehudumu katika nafasi hiyo
kwa siku 263 tangu alipoteuliwa mpaka leo uteuzi wake ulipotenguliwa na
Rais magufuli.
Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchapa kazi kwa bidii kwani mpaka sasa bado utendaji wao bado unasuasua.
Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchapa kazi kwa bidii kwani mpaka sasa bado utendaji wao bado unasuasua.
No comments:
Post a Comment