Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema wanamuonea wivu waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa kwa
kupata nafasi ya kuongea na Rais John Magufuli.
Lowassa
jana Jumanne alitembelea Ikulu ya Dar es Salaam na kufanya mazungumzo
na Rais Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine alimpongeza Rais kwa
jitihada zake za kuleta maendeleo na ajira kwa vijana.
Hatua
hiyo ya Lowassa ilikosolewa na baadhi ya viongozi wakubwa wa chama
chake wakieleza kuwa hakutakiwa kutoa pongezi kwa Rais huyo kwa kuwa
uongozi wake una kasoro huku wakiuambia umma kwamba maneno ya Lowassa ni
ya kwake binafsi na sio msimamo wa chama chake.
Gambo
ambaye awali alijinadi kuwa Lowassa anamuomba amuombee nafasi ya
kuonana na Rais, amesema wanaokosoa wanafanya hivyo kwa kuwa wao
hawajabahatika.
"Lowassa
alikuwa na kiu ya muda mrefu kutaka kumuona Rais hatimaye Rais
amemaliza kiu hiyo. Mbowe na Lema nao kama watu wenye akili timamu bila
shaka nao wanayo kiu ya kuonana na kiongozi mkuu wa nchi, hivyo niwatake
wafuate taratibu na kama Rais atakuwa na nafasi ataonana nao hana shida
katika hilo," amesema Gambo.
Amesema
Rais ameonyesha mfano wa siasa safi na vijana wanapaswa kuiga mfano
wake kwani baada ya uchaguzi agenda yake kubwa ni maendeleo.
Alipoulizwa
kuwa tukio la jana ni matokeo ya matamshi yake ya kutumwa na Lowassa
ambayo baadaye Lowassa mwenyewe aliyakana, Gambo amesema "Ninaloweza
kusema ni Rais kamaliza kiu ya muda mrefu."
Kuhusu
kama kweli ujumbe huo aliufikisha kwa Ikulu kwa Rais Magufuli Gambo
amesema " Mawasiliano ya Rais na Mkuu wa Mkoa si jambo la umma hivyo
nisilizungumzie,"
No comments:
Post a Comment