WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na usafirishaji wa mbolea
kutoka wa wasambazaji wa pembejeo nchini kwenda kwa wakulima.
Pia ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuwa na mikakati madhubuti itakayowezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati wote nchini.
Ametoa
kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati akikagua
usafirishaji wa mbolea kwenye maghala makubwa matatu jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata
pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuwaletea
tija.
Amesema
TFC inatakiwa ianze maandalizi ya usambazaji wa mbolea mapema kwani
Serikali inataka wakulima wapate pembejeo miezi miwili kabla ya kuanza
kwa msimu.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba
akutane na wadau na kufanya mapitio ya gharama za usafirishaji wa
mbolea.
Amesema
lengo la mapitio hayo ni kuhakikisha mkulima aliyeko kijijini anapata
mbolea hiyo kwa gharama nafuu bila ya kumuathiri mfanyabiashara.
Pia
amemtakaDkt. Tezeba ashirikiane na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Dkt. Mwigulu Nchemba ili kuhakikisha malori yanayobeba mbolea yanafika
katika mikoa husika kwa wakati.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo awasiliane na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawala ili malori
yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele.
“Si
kwamba yaongeze uzito hapana, bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka
ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza.”
Naye
Waziri wa Kilimo, Dkt. Tizeba alisema watahakikisha mbolea ya kutosha
inakuwepo nchini na kwamba wakulima wote wanaipata kwa wakati na kwa
gharama nafuu.
Maghala
aliyoyakagua Waziri Mkuu ni ghala la Mohammed Enterprises lililoko
Mbagala, ghala la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililoko Kurasini na
ghala la Premium lililoko Vingunguti ambako kote amekuta malori
yakipakia mbolea kwa ajili ya uisafirisha katika mikoa mbalimbali
nchini.
No comments:
Post a Comment