Wanahabari
wanne wa vyombo mbalimbali vya habari wilaya ya Kahama wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujipatia Sh1milioni kutoka kwa mganga wa
jadi baada ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa.
Akizungumza
leo Januari 10, 2018 Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule
amewataja waandishi hao na vyombo vyao katika mabano kuwa ni Paul
Kayanda (gazeti la Uhuru), Shaban Njia (Nipashe), Simon Dionis (Radio
Kwizera) na Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo, huku mmoja
akikimbia.
Amesema
watuhumiwa hao walitenda kosa hilo jana Januari 9 saa 7 mchana katika
kitongoji cha Ng’wande kijiji cha Bani wilayani Kahama baada ya
kumtishia mganga huyo, Jane Mbeshi (46) kuwa wao ni maofisa usalama
kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kagera, Shinyanga na Kahama.
Amebainisha
kuwa baada ya kujitambulisha, walimtaka mganga huyo kuwapa kiasi cha
Sh2 milioni ili wasimtie mbaroni kwa kosa la kupiga ramli chonganishi.
“Januari
6 watuhumiwa walipokea Sh1 milioni kutoka kwa mganga huyo kwa
makubaliano kuwa kiasi kingine kilichosalia wangepewa siku nyingine,”
amesema Haule na kuongeza,
“Baada
ya kupokea taarifa hizo polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwatia
mbaroni watuhumiwa watatu kati ya watano waliofika nyumbani kwa mganga
huyo kupokea kiasi cha fedha kilichosalia.”
Amesema
waliokamatwa kwenye eneo la tukio ni Kayanda, Njia na Dionis huku
Mihayo akijisalimisha mwenyewe polisi jana, kwamba mtuhumiwa wa tano,
George Maziku anaendelea kusakwa na polisi.
No comments:
Post a Comment