Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amesema kuwa hana mpango wa kuhamia chama
chochote cha upinzani na ataendelea kubaki ndani ya CCM.
Alisema
hawezi kufanya uamuzi wa kuhamia katika vyama vya upinzani , huku
akidai magari ya upinzani kwa sasa yanazidi kuzama na haijulikani
yataibuka lini.
Kauli
hiyo aliitoa mjini Songea wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Songea
kupitia CCM, DK. Damas Ndumbaro katika mkutano wa kampeni uliofanyika
kata ya Bombambili mjini hapa.
Nape
ambaye pia aliwahi kuwa katibu Mwnezi wa CCM, alisema kama kuna watu
walidhani atakihama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani wasahau.
Alisema matatizo ya chama humalizwa ndani ya chama na si kukihama kama walivyofanya wanachama wengine waliokimbia ndani ya CCM.
“Naikubali
serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari DK. John Magufuli
pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu,
Kassimu Majaliwa. Ni serikali yenye viongozi imara na mimi naapa kufia
CCM na sivinginevyo.
“Nasikia
maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia
upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na
mawazo hayo,” alisema Nape
No comments:
Post a Comment