Pages

Tuesday, December 26, 2017

Ballon d'Or: Nani atakayeshinda tuzo hiyo baada ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi?


Neymar, Kylian Mbappe, Kevin de Bruyne, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi
Wawili hao wameonyesha uwezo wao wa kuwa wachezaji bora duniani kwa takriban muongo mmoja, wakishikilia mataji yaa mchezaji bora kitu ambacho hakijawahi kufanyika miaka iliopita na hakitafanyika tena katika siku zijazo.
Mchezo wao mzuri umewafanya kutuzwa mataji mengi huku Messi anayeichezea Barcelona akishinda mataji matano ya Ballons d'Or, ikiwa ni moja zaidi ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Lakini ni nyota wapi wa soka watakaowarithi wachezaji hao wawili. Tuliwauliza wataalam wa soka wa BBC kutoa uamuzi wao.

Nyota ya mchezaji De Bruyne imeanza kung'aa
Mchezaji huyo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne pamoja na mwenzake wa Chelsea Eden Hazard ndio wachezaji katika ligi ya Uingereza wanaopigiwa upato kushindania taji la Ballon d'Or wakati utawala wa Messi na Ronaldo utakapofikia kikomo.
De Bruyne, 26, amekuwa mchezaji bora msimu huu na huku mchezaji huyo wa Ubelgiji akiwa hajafikia kiwango cha wawili hao nyota yake imeanza kung'aa
Mpinzani wa De Bruyne anaweza kuwa mchezaji mwenza wa Chelsea Eden Hazard, ambaye pia ana umri wa 26, ambaye mchezo wake msimu huu kufuatia uwezo wake wa kuisadia Chelsea kushinda taji la ligi ya Uingereza pia umemfanya kuwa mwananiaji wa tuzo hilo siku zijazo.
Mshambuliaji wa City Gabriel Jesus ambaye ana umri wa miaka 20 pia huenda akaonekana kuwa mgombea wa tuzo hilo huku kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba pia akionekana kuudhibiti ulimwengu katika miguu yake.
Wachezaji wa Tottenham Harry Kane na kiungo wa kati Dele Alli pia watajiimarisha miongoni mwa wachezaji bora wa Ulaya huku mchezaji wa Liverpool Phillipe Coutinho ,25, akidaiwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa soka duniani.
Na iwapo tunaangazia nyota inayoendelea kung'aa ambaye huenda akatawazwa katika siku za usoni ,basi tusimsahau mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah? Ana umri wa miaka 25 na amekuwa mchezaji bora tangu uhamisho wake kutoka Roma wa £34.5m.
Ballon d'Or-Miaka ambayo Messi na Ronaldo walishinda tuzo hiyo
2008 Cristiano Ronaldo Lionel Messi Fernando Torres
2009 Lionel Messi Cristiano Ronaldo Xavi
2010 Lionel Messi Andres Iniesta Xavi
2011 Lionel Messi Cristiano Ronaldo Xavi
2012 Lionel Messi Cristiano Ronaldo Andres Iniesta
2013 Cristiano Ronaldo Lionel Messi Franck Ribery
2014 Cristiano Ronaldo Lionel Messi Manuel Neuer
2015 Lionel Messi Cristiano Ronaldo Neymar
2016 Cristiano Ronaldo Lionel Messi Antoine Griezmann
Neymar anakabiliwa na shinikizo ya kuipatia PSG kombe la vilabu bingwa
Tuanze na mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar - ambaye ndiye mchezaji bora wa soka ya Brazill tangu 2011 , na mtu ambaye anaweza kuwa mshindi wa kwanza wa taji la Ballon d'Or kutoka Brazil tangu Kaka 2007.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ndio kiongozi wa timu yake na mchezaji mwenye thamani kubwa duniani.
Katika mashindano ya kombe la dunia la 2014 ndio mchezaji ambaye Brazil walimtegemea sana na dunia ilijionea timu yake ilivyocheza vibaya alipotoka katika timu hiyo.
Sasa yuko imara zaidi .Lakini ana changamoto kubwa baada ya kujiunga na PSG kwa sababu alinunuliwa ili kuishindia timu hiyo kombe la vilabu bingwa na iwapo atashinda itaonekana kwamba ameshindwa.
Neymar ni mfalme wa kutoa pasi zinazosababisha magoli
Neymar alitoa pasi 22 kwa Messi ikilinganishwa na mchezaji yeyote yule wakati alipokuwa akiichezea klabu hiyo.
Iwapo utakiangazia kikosi cha Brazil , hakuna wachezaji wengi kama yeye .
Jesus ana uwezo na ana mkufunzi hodari wa kumwezesha kufika katika kiwango cha mchezaji bora kupitia Pep Guardiola lakini hilo huenda lisiafikiwe hivi karibuni.
Mchezaji wa Brazil anayefanya vizuri Ulaya kwa sasa ni Ederson-lakini kipa hajawahi kushinda taji hilo tangu Lev Yashin mwaka 1963.
Kuna habari nyingi za sifa kumhusu mshambuliaji wa Flamengo mwenye umri wa miaka 17 Vinicius, lakini hajafanya lolote kuthibitisha hilo ijapokuwa ana kandarasi na Real Madrid.
Mshambuliaji wa Gremio Luan mwenye umri wa miaka 24 ana kitu tofauti, lakini timu za Ulaya zilikuwa zikimchunguza na kuamua kutomsajili.
Iwapo Neymar atashinda taji la Ballon d'Or, atakuwa mchezaji wa kwanza wa Brazil ambaye jina lake halianzi na R- baada ya Ronaldo, Ronaldinho na Ricky Kaka.
Mbappe ana uwezo mkubwa wa kuwa mchezaji bora duniani
Wakati nilipoitembelea klabu ya kwanza ya Kyllian Mbappe, AS Bondy, mapema mwaka huu , wakufunzi wake walianiambia kwamba wamekuwa wakimuita mshindi wa siku zijazo wa Ballon D'Or tangu alipokuwa akiitembelea klabu hiyo katika umri wa miaka saba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alionyesha umahiri wake msimu uliopita alipoifungia Monaco mabao 26, na sasa ana uwezo mkubwa wa kuwa mchezaji bora duniani.
Mwaka ujao , Mbappe atakuwa mchezaji wa pili mwenye thamani duniani wakati Paris St-Germain itakapompatia mkataba wa kudumu na mchezaji atakayekuwa katika nafasi ya tatu - Ousmane Dembele - anaweza kuwa mpinzani wake mkuu katika kipindi cha muongo mmoja ujao.
Jeraha la nyuma ya goti limemzuia Dembele, 20, kuwaonyesha mashabiki wa Barcelona kile anachoweza kufanya , lakini alionyesha katika klabu ya Rennes na Borussia Dortmund kwamba ana kila uwezo wa kuwa mchezaji bora duniani.
Huu hautakuwa upinzani kati ya Messi na Ronaldo, - Mbappe na Dembele ni marafiki wakubwa na wataichezea safu ya mashambulizi ya Ufaransa katika kipindi kirefu kijacho
Ronaldo dhidi ya Messi

Ronaldo Messi
Mechi 471 396
dakika walizocheza 38,251 31,798
Mabao 371 362
Mashambulizi 2,692 1,735
Viwango vya mashambulio yaliosababisha magoli 13.8% 20.9%
Dakika kwa kila bao 103.1 87.8
'Keita ana siku njema zijazo

Iwapo Mwafrika atashinda taji la Ballon d'Or siku zijazo au la itategemea na mkufunzi wa Ujerumani - Jurgen Klopp.
Wachezaji wa Afrika wenye thamani ya juu , wale walio na uwezo wa kuimarika watakuwa wakicheza katika kikosi cha Jurgen Klopp na Liverpool katika kipindi cha miaka michache ijayo - mchezaji wa Misri Salah, mchezaji wa Senegal Sadio Mane na mchezaji wa Guinea Naby Keita.
Salah alivyoanza vyema
Mohamed Salah amehusika katika mabao 15 katika mechi zake 15 za ligi ya Uingereza akiichezea Liverpool - ikiwa ni zaidi ya mchezaji mwengine yeyote wa klabu hiyo . (Amefunga mabao 12 na kutoa pasi 3 zilizosababisha mabao).
Wachezaji wote watatu tayari wameonyesha kwamba wana uwezo mkubwa katika klabu yao.
Salah na Mane ambao wote wana umri wa miaka 25 pia wana uwezo wa kuwa viungo muhimu katika timu zao za kitaifa wote wakiwa tayari kuzichezea timu zao katika kombe la dunia msimu ujao.
Wote wawili wamebarikiwa na kasi na wanaimarisha uwezo wao wa kufunga mabao -iwapo hilo litaendelea wanaweza kuwa na sifa ya kuwa wachezaji bora duniani.
Keita ndiye mchezaji ambaye ameisaidia klabu ya RB Leipzig kuimarika katika ligi ya Bundesliga na anatarajiwa kuimarika katika kikosi bora na katika ligi yenye ushindani mkubwa akiichezea in a stronger squad and in a more competitive league at Liverpool.
Iwapo atavaa viatu vya mchezaji wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard, basi atatuzwa duniani.
Akiwa na uwezo wa kulinda lango kama vile N'Golo Kante na uwezo wa kufanya mashambulio anaweza kutengeza magoli na kufunga, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ana siku bora za usoni.

No comments:

Post a Comment