
Wakati huohuo manchester United imeimarisha dau lake kwa kiungo wa kati Marouane Fellaini, ili kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye I yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu (Daily Express)
Arsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain. (Mirror)
Hatahivyo usajili wa mchezaji huyo wa hadi £35m utaifanya Arsenal kumuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 29, mnamo mwezi Januari. (Daily Mail)
Mkufunzi mpya wa West Ham David Moyes ana hamu ya kumsajili Steven Nzonzi iwapo Sevilla itaamua kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 mwaka ujao. (Guardian)
Mkufunzi Roy Hodgson anahofia kwamba Crystal Palace italazimika kumuuza Wilfried Zaha mwezi ujao huku Manchester City, Chelsea na Tottenham zote zikimtaka winga huyo ,25, (mirror)
Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce amefichua kwamba aliisaidia kuimarisha motisha ya mabeki Michael Keane na Ashley Williams kupitia usaidizi wa mchezo wa runinga wa The Cube. (Liverpool Echo)
No comments:
Post a Comment