Pages

Tuesday, December 26, 2017

BARA YAAMKA SOKA LA UFUKWENI NA KUIZAMISHA ZANZIBAR KWA MABAO 4-0


Baada ya kupoteza dhidi ya Malawi, Tanzania Bara imeamka na kuitwanga Zanzibar kwa mabao 4-3 katika michuano ya Copa Dar es Salaam inayoendelea katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ilikuwa na ushinda baada ya timu zote kuwa zimecheza mechi moja moja na Bara walikuwa wamepoteza dhidi ya Malawi na Zanzibar walikuwa wameshinda dhidi ya Uganda.

Zanzibar walianza hasa kipindi cha kwanza lakini mwishoni walionekana kupoteza hali ya nidhamu ya mchezo na kuwaruhusu Bara kutawala na kupachika mabao ya harakaharaka.

Michuano hiyo ya soka la ufukweni kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Malawi wakiwa wamealikwa, imekuwa kivutio kikubwa leo.

No comments:

Post a Comment