Pages

Tuesday, December 26, 2017

MSHAMBULIAJI MPYA WA SIMBA AOTA MBAWA, RAIS WAKE AMZUIA KUREJEA


Pamoja na kumsajili mshambuliaji Dayo Domingues na kukamilisha kila kitu, Simba imeshindwa kumpata.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Msumbuji ameshindwa kurejea baada ya Rais wa klabu ya Ferreviario kuweka ngumu.


“Rais wa timu hiyo amesema pamoja na klabu, yeye ana mkataba naye binafsi hivyo hawezi kuja Tanzania,” kimeeleza chanzo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Simba imekuwa ikifanya juhudi kupata mawasiliano ya rais huyo na kama itashindikana itaendelea kubaki na kumpa nafasi nyingine Laudit Mavugo.

No comments:

Post a Comment